Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 23:39

Kremlin yasema mazungumzo ya amani juu ya Ukraine bila Russia 'hayana maana'


Kutoka kushoto: Rais wa Russia Vladimir Putin na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy.
Kutoka kushoto: Rais wa Russia Vladimir Putin na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy.

Msemaji wa rais wa Russia Dmitry Peskov amesema leo kwamba mazungumzo ya amani ya Ukraine bila Moscow hayana maana.

Pesvoc alikuwa anajibu kuhusu pendekezo la Uswis kuanda Mkutano wa maafisa waandamizi wa kimataifa mwezi juni kusaidia kutengeneza njia ya amani Ukraine baada ya miaka miwili ya mapigano.

Mkutano umepangwa kufanyika Juni 15 – 16 ambapo utawakutanisha maafisa wa serikali kutoka dazani za nchi, kufuatia mpango uliowasilishwa miezi ya karibuni na rais wa Ukraine Volodymir Zeelensky na waziri wa mambo ya nje wa swiss Ignazio Cassis.

Pescov alisisitiza kwamba “ tumesema mara nyingi kwamba mazungumzo bila Russia hayana maana.

Dmintry Peskov, msemaji wa rais wa Russia, Vladmir Putin asema: “Rais Putin amesisitiza kwamba bado tuko wazi kwa ajili ya mazungumzo. Mchakato huu ni njia bora zaidi ya kufikia malengo yetu . lakini kutokana na kwamba wa-ukraine wamekataa kushiriki katika mazungumzo hatuoni matarajio yoyote.”

Wakati huo huo Rais Zelensky wa Ukrain aliwasili Vilnius, Lithuania kwa mazungumzo ya viongozi wa vnchi za Ulaya ya kati na mashariki juu ya kuisaidia nchi yake iliyoharibiwa na vita. Zelensky anaomba mfumo mpya wa ulinzi wa angaambayo anasema ndio kipaumbele cha kwanza cha Kyiv.

Forum

XS
SM
MD
LG