Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 24, 2024 Local time: 01:36

Ukraine itashindwa katika vita vyake dhidi ya Russia ikiwa haitapata msaada wa dola bilioni 60 kutoka kwa Marekani-Zelenskiy


Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy akizungumza na spika wa Bunge la Marekani Mike Johnson kwa njia ya simu, mjini Kyiv, Machi 28, 2024.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy akizungumza na spika wa Bunge la Marekani Mike Johnson kwa njia ya simu, mjini Kyiv, Machi 28, 2024.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy Jumapili alisema kwamba Ukraine itashindwa katika vita vyake dhidi ya Russia ikiwa Bunge la Marekani halitaidhinisha msaada mkubwa wa kijeshi, huku wanajeshi wa Russia wakiendelea kujiimarisha kwenye uwanja wa mapambano.

Jeshi la Ukraine limekiri kuwa mapigano karibu na mji wa Chasiv Yar yamekuwa “magumu” na “makali” lakini limesisitiza kuwa wanajeshi wake wamesimama imara.

Huku pande zote zikifanya mashambulizi ya anga, Russia ilisema kuwa ndege moja isiyo na rubani ya Ukraine ilishambulia kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia ambacho imekikalia tangu muda mfupi baada ya kuanzisha uvamizi wake mwaka 2022.

Ukraine imekuwa ikitoa wito wa dharura kwa Marekani kuanza kuwasilisha muswada wa dola bilioni 60 ambao umekwamishwa na Warepublican katika Baraza la Wawakilishi kwa miezi kadhaa.

“Ni muhimu kuliambia Bunge hasa kwamba ikiwa halitaisidia Ukraine, Ukraine itashindwa vita,” Zelenskiy alisema katika mkutano kwa njia ya video.

Itakuwa vigumu kwa Ukraine kusimama imara bila msaada huo, Zelenskiy aliongeza. “Ikiwa Ukraine itashindwa vita, mataifa mengine yatashambuliwa.”

Forum

XS
SM
MD
LG