Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amewataka washirika wa magharibi siku ya Jumatatu kuiruhusu Kyiv kushambulia malengo ya kijeshi ndani ya Russia kwa kutumia silaha za masafa marefu za mataifa ya magharibi katika kujilinda.
“Tunahitaji kuimarisha kazi yetu ya pamoja na washirika wetu ili kufanikisha zaidi. Usalama na kulazimishwa Russia kuimarisha amani kwa njia zote”, Zelenskyy aliwaambia waandishi wa habari na Waziri Mkuu wa Uhispania, Pedro Sanchez wakati wa ziara huko Madrid siku ya Jumatatu.
“Tunahitaji kufanya kazi pamoja na kuweka shinikizo sio tu kwa Russia, lakini pia kwa washirika wetu kutupa fursa ya kujilinda dhidi ya Russia”, Zelensky alisema, akiongeza kuwa Ukraine inahitaji mifumo ya ulinzi wa anga ili kujilinda dhidi ya mashambulizi ya anga ya Russia. Wakati wa ziara yake mjini Sofia, Bulgaria, siku ya Jumatatu, mkuu wa NATO Jens Stoltenberg aliunga mkono matamshi ya Zelenskyy.
Aliwaomba maafisa wa NATO kufikiria upya vikwazo vyao dhidi ya Kyiv kwa kutumia silaha za Magharibi kushambulia ndani ya Russia, akisema kuwa Ukraine ina haki ya kujilinda, ikijumuisha kushambulia “malengo halali nje ya Ukraine”.
Forum