Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 03, 2025 Local time: 06:51

Trump asema ameanza mazungumzo na Putin na Zelenskiy kumaliza vita vya Ukraine


Rais Donald Trump, Rais Volodymyr Zelenskiy na Rais Vladimir Putin
Rais Donald Trump, Rais Volodymyr Zelenskiy na Rais Vladimir Putin

Rais Donald Trump Jumatano alitangaza kwamba yeye na Rais wa Russia Vladimir Putin wamekubaliana katika mazungumzo ya simu “kuanza mara moja” mazungumzo na kiongozi wa Ukraine ili kumaliza mzozo wa karibu miaka mitatu.

Rais Trump baadaye alizungumza kwa njia ya simu na Rais Volodymir Zelensky wa Ukraine. “Nimekuwa na mazungumzo yenye tija na Rais Zelensky,” Trump aliwaambia waandishi wa habari Jumatano jioni katika Ikulu hapa Washington DC, bila kutoa maelezo zaidi.
‘Nimemuomba waziri wa mambo ya nje Marco Rubio, mkurugenzi wa CIA John Ratcliffe, Mshauri wa usalama wa taifa Michael Waltz, na Balozi na Mjumbe Maalum Steve Witkoff, kuongoza mazungumzo ambayo, ninahisi kwa dhati, yatakuwa na mafanikio.”

Trump hakufafanua ni masharti gani ambayo yatapelekea kumaliza mzozo huo kati ya Russia na Ukraine.

Forum

XS
SM
MD
LG