Lake ambaye amekuwa mwanahabari kwa miaka 30 alitangazwa na Rais Donald Trump mwezi Desemba kama mtu ambaye angependa aiongoze Sauti ya Amerika (VOA).
Hata hivyo uteuzi wa Lake kwa nafasi hiyo umekawia wakati mteuliwa wa Trump wa kuongoza USAGM mkonsavative, mwanaharakati wa siasa na pia mwandishi L.Brent Bozell III anasuburi kuidhinishwa na Seneti.
Shirika hilo la USAGM pia linasubiri kupata bodi mpya isiyoegemea upande wowote, ambayo itafanya kazi na mtendaji mkuu kwenye masuala ya kuwateua au kuwafukuza kazi wakuu wa vituo vya matangazo.
Roman Napoli ambaye anakaimu nafasi ya mkurugenzi mtendaji mkuu wa USAGM aliyeondoka Amanda Bennet, kupitia barua pepe kwa wafanyakazi, alitangaza ujio wa Lake.
“Lake analeta uzoefu mkubwa kwenye uandishi wa habari, baada ya kuwa mtangazaji na mwanahabari kwa zaidi ya miongo miwili kwenye mashirika makubwa ya habari,” Napoli alisema.
Akiangazia mafanikio yake, Napoli alisema kuwa Lake aliwahi kuwahoji viongozi, pamoja na marais wawili wa Marekani, na pia kupewa tuzo za Emmy mara mbili kutokana na utangazaji wake wa kimataifa.
Forum