Aidha, Trump alisema kwenye mtandao wake wa kijamii Truth Social kwamba ataiwekea China ushuru mwingine wa asilimia 10 Jumanne ijayo kwenye bidhaa zake inazouza Marekani, kuongeza kwenye ushuru wa asilimia 10 alioweka mapema mwezi huu.
China iliweka kwa haraka ushuru sawa na ule wa kwanza wa Trump kwenye bidhaa za Marekani.
“Dawa za kulevya bado zinaingia kwa wingi nchi mwetu kutoka Mexico na Canada kwa viwango vya juu na visivyokubalika,” Trump alisema.
“Kiwango kikubwa cha dawa hizi, nyingi zikiwa aina ya Fentanyl, zinatengenezwa China na kusafirishwa na nchi hiyo.”
Trump alitangaza kwanza ushuru kwenye bidhaa za Canada na Mexico, washirika wawili wa karibu wa Marekani na washirika wa kibiashara, mapema mwezi huu.
Forum