Nchini Saudi Arabia waatalamu wa masuala ya mwezi na sayari walikuwa katika kituo cha kufuatilia sayari na mwezi katika mji wa kusini wa Hautat Sudir siku ya Ijumaa ili kuutafuta mwezi wa siku ya kwanza kwa kutumia vyombo vya kisasa.
Katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) maafisa wa kidini wametumia ndege zisizo na rubani na akili mnemba AI ili kuutafuta mwezi, ikiwa ni mara ya kwanza kutumia teknolojia hiyo mpya duniani.
Wakuu wa dini wanasema teknolojia hiyo itatumiwa ili kusaidia kukamilisha utaratibu wa kuuona mwezi kwa macho.
Kulingana na kanuni za kislamu siku ya kwanza ya Ramadhani huanza baada ya mwezi kuandama siku moja kabla na kuonekana na mtu wa kuaminika na mashahidi wawili.
Katika mji mkuu wa Jakatra, Indonesia waislamu walianza swala ya Taraweh ambayo hufanyika mnamo mwezi kamili wa Ramadhan.
Huo kwenye mji wa Nuseirat, Ukanda wa Gaza na Gaza City wafanyakazi na malori yameonekana yakiondoa vifusi wakati mji unajitayarisha kwa mwezi wa Ramadhan.
Nabil al-Salihi meya wa Nuseirat anasema "kampeni hii ilianzishwa na serikali za manispaa za Ukanda wa Gaza tunapouanza mwezi wa Ramadhani. Ikiwa na ujumbe wa 'Gaza hupendeza zaidi wakati wa Ramadhani’, ambao una lengo la kuona tabasamu kwenye sura za wakazi wanaostahili kushukuriwa na kupongezwa kwa subra waliyokuwa nayo."
Hali kadhalika tunatoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kuingilia kati kutekeleza makubaliano ya kuwasilisha huduma za dharura na kuruhusu vifaa vinavyohitajika kuondoa vifusi vikubwa.
Kundi la Hamas nalo limetoa wito wa kuongezwa muda wa makubaliano ya kusitisha mapigano mnamo mwezi huu wa Ramadhani wakati mazungumzo ya awamu ya pili yanapoanza Ijumaa mjini Cairo.
Nao wakazi wa mji wa Port Sudan, nchini Sudan wamekuwa wakijitayarisha kwa mwezi mtukufu wakati vita vikiendelea kati ya jeshi la taifa linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan na naibu wake wa zamani Mohamed Hamdan Daglo anayeongoza kundi la wanamgambo la RSF.
Watu wanalalamika kupanda kwa bei za bidhaa muhimu na mara nyingi hazipatikani.
Hali kama hiyo ina wakumba wakazi wa Yemen ambao wanashuhudia utulivu hivi sasa baada ya vita vya karibu muongo mmoja.
Waleed al-Sofi meneja wa duka kubwa la biashara katika mji wa Sanaa anasema watu wananunua kulingana na uwezo wao kuanzia dola 30 hadi dola 200.
Ripoti hii inatokana na mkusanyiko wa habari kutoka Reuters na AFP.
Forum