Waziri wa maendeleo ya kimataifa wa Autralia Pat Conroy, ameambia waandishi wa habari katika mji mkuu wa Port Vila nchini Vanuatu kwamba Australia itaendelea kusaidia nchi hiyo.
Conroy, ambaye amefanya mazungumzo na Waziri mkuu wa Vanuatu Jotham Napat, ameahidi msaada kwa bajeti ya Vanuatu, wa kiasi cha dola milioni 3.2, baada ya kutokea tetemeko la ardhi mwezi Desemba lililoharibu nyumba kadhaa na kusababisha vifo vya watu 16.
Conroy amesema kwamba nchi kubwa zinashindana kuwa na ushawishi katika kanda hiyo lakini Australia inajivunia kuwa mshirika mkubwa wa maendeleo, akisisitiza kwamba nchi hiyo ilikuwa inatoa msaada kwa nchi za kanda ya Pacific kabla ya nchi nyingine, ikiwemo Marekani, au China.
Forum