Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Machi 30, 2025 Local time: 23:10

SWAPO ilishinda uchaguzi wa Namibia kihalali - Mahakama ya juu


Rais Mteule wa Namibia Netumbo Nandi-Ndaitwah baadaya kupiga kura yake huko Windhoek, Namibia, Novemba 27, 2024. Picha na REUTERS/Noah Tjijenda
Rais Mteule wa Namibia Netumbo Nandi-Ndaitwah baadaya kupiga kura yake huko Windhoek, Namibia, Novemba 27, 2024. Picha na REUTERS/Noah Tjijenda

Mahakama ya Juu ya Namibia siku ya Ijumaa ilitupilia mbali pingamizi dhidi ya uchaguzi wa rais wa mwaka jana lililowasilishwa na vyama vya upinzani, hatua ambayo inampa nafasi Netumbo Nandi-Ndaitwah wa chama kinachotawala, kuwa rais kuanzia mwezi ujao.

Chama cha SWAPO cha nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika, ambacho kimetawala taifa hilo la watu milioni 3 kwa zaidi ya miongo mitatu, kilishinda uchaguzi wa rais na bunge mwezi Novemba.

Vyama vya upinzani vilidai uchaguzi huo ulikuwa na dosari na kwa hivyo batili, kutokana na kuongezwa muda wa kupiga kura kwa siku kadhaa, miongoni mwa masuala mengine.

Jaji Mkuu wa Namibia Peter Shivute aliamua kuwa uamuzi wa kuongeza muda wa upigaji kura ulikuwa halali na kutupilia mbali changamoto iliyoletwa na Chama Huru cha Wazalendo wa Mabadiliko (IPC), ambacho kilishika nafasi ya pili katika uchaguzi huo.

Katika kesi yake, IPC iliungana na chama kingine cha upinzani, Landless People's Movement.

Kiongozi wa IPC na mgombea urais mwaka jana, Panduleni Itula, alisema chama chake kitaheshimu uamuzi huo."Hatuendi mitaani kuandamana au kitu kama hicho," Itula alisema.

Nandi-Ndaitwah ataapishwa kama rais wa kwanza mwanamke wa Namibia Machi 21.

Forum

XS
SM
MD
LG