Kenya imetangaza kuwa inahitaji bilioni 24.9 kukidhi huduma za afya baada ya Marekani kusitisha misaada
Rubio yupo Saudi Arabia huku kukiwa na upinzani kuhusu pendekezo la Rais wa Marekani Donald Trump la kuwaondoa Wapalestina kutoka Gaza
Viongozi wa Umoja wa Ulaya katika siku za hivi karibuni wameahidi kuendelea kuiunga mkono Ukraine akiwemo Waziri Mkuu wa Uingereza.
Walioshuhudia tukio waliliambia shirika hilo la habari la serikali kuwa mlipuko wa mitungi ya gesi ulisababisha kuanguka kwa jengo hilo
Serikali ya Uganda Jumapili ilisema itaiondoa kesi dhidi ya mpinzani mkongwe Kizza Besigye katika mahakama ya kijeshi, na kumtaka asitishe mgomo wa kula gerezani, waziri mmoja amesema.
Nyota wa muziki, raia wa Colombia Shakira, Jumapili amelazimika kusitisha show yake huko Lima, Peru, na baadaye kupelekwa hospitalini kutokana na maumivu ya tumbo.
Mahakama ya Mauritius imemuachilia kwa dhamana Waziri Mkuu wa zamani Pravid Jugnauth, baada ya kukamatwa Jumamosi kwa tuhuma za usafirishaji haramu wa fedha, baada ya masanduku yaliojaa fedha kupatikana kwake nyumbani kufuatia msako.
Mke wa kiongozi wa upinzani nchini Uganda aliye chini ya ulinzi Kizza Besigye, Jumapili amesema ana wasiwasi kuhusu afya yake, ikiwa karibu wiki moja baada ya mgombea huyo wa zamani wa urais kuanza mgomo wa kula.
Baadhi ya Wazungu wa Afrika Kusini, Jumamosi walionyesha kumuunga mkono Rais Donald Trump, kwa kukusanyika katika Ubalozi wa Marekani mjini Pretoria kudai wao ni waathirika wa ubaguzi wa rangi na serikali yao wenyewe.
Wanajeshi wa Russia, wameongeza kasi ya mashambulizi yao mashariki mwa Ukraine, jeshi la Kyiv, limesema Jumapili, huku afisa wa NATO akitabiri kuwa Moscow itaongeza kasi na nguvu ya mashambulizi yake wakati mazungumzo ya kumaliza vita yanakaribia.
Katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia, viongozi wa Afrika wamemchagua Waziri wa Mambo ya Nje wa Djibouti, Mahmoud Ali Youssouf, kuwa Mwenyekiti mpya wa Tume ya Umoja wa Afrika (AUC).
Pandisha zaidi