Polisi walimzuilia kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 63 pamoja na mke Kobita Jugnauth huku wakihojiwa kwa saa kadhaa Jumapili asubuhi. Kobita aliachiliwa muda mfupi baadaye huku Pravid akiendelea kushikiliwa.
Alikanusha shutuma zote dhidi yake baada ya kufikishwa mahakamani kwenye mji mkuu wa Port Louis. Baadaye jaji alimwachilia kwa dhamana ya dola 16,000 za Kimarekani, kupitia uamuzi uliyoonyeshwa shirika la habari la AP. Pravind Jugnauth alikuwa waziri mkuu wa Mauritius kuanzia 2017 hadi 2024, na ametokea kwenye moja wapo ya familia ambazo zimekuwa kwenye utawala wa taifa hilo la kisiwa lilipo kwenye bahari Hindi tangu kujipatia uhuru wake kutoka kwa Uingereza 1968.
Yeye alisimamia mkataba wa kihistoria kati ya Uingereza na Mauritius wa kuchukua tena udhibiti wa visiwa vya Chagos vilivyozozaniwa kwa muda mrefu. Hata hivyo yeye na chama chake cha Militant Socialist Movement walishindwa vibaya kwenye uchaguzi wa Novemba uliyokuwa na ushindani mkali. Nafasi yake ilichukuliwa na Navin Ramgoolam mwenye msimamo wa kushoto kati akifanyika waziri mkuu kwa mara ya tatu.
Forum