Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 03, 2025 Local time: 00:39

Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani yupo Saudi Arabia anakutana na MBS


Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio (L) akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Prince Faisal bin Farhan Al Saud mjini Riyadh, Saudi Arabia. Feb. 17, 2025.
Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio (L) akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Prince Faisal bin Farhan Al Saud mjini Riyadh, Saudi Arabia. Feb. 17, 2025.

Rubio yupo Saudi Arabia huku kukiwa na upinzani kuhusu pendekezo la Rais wa Marekani Donald Trump la kuwaondoa Wapalestina kutoka Gaza

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio alikuwa nchini Saudi Arabia leo Jumatatu kama sehemu ya ziara ya eneo hilo ambayo inajumuisha kulenga usitishaji mapigano kati ya Israel na Hamas.

Rubio alitarajiwa kukutana na Mwanamfalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman huku kukiwa na upinzani kutoka Saudi Arabia na mataifa mengine ya Kiarabu kuhusu pendekezo la Rais wa Marekani Donald Trump la kuwaondoa Wapalestina kutoka Gaza. Trump anapendekeza kuwa Wapalestina watakwenda katika nchi jirani huku Marekani ikiichukua Gaza na kuliendeleza eneo hilo.

Mpango kama huo unaonekana kuondoa matumaini ya Trump ya kuipata Saudi Arabia kurejesha uhusiano na Israel hatua ambayo maafisa wa Saudi Arabia wanasema haitatokea, isipokuwa kama kuna njia ya kuundwa kwa taifa la Palestina.

Marekani iliidhinisha kikamilifu malengo ya vita vya Israel huko Gaza siku ya Jumapili, huku Rubio akisema kuwa Hamas lazima litokomezwe na hawawezi kuendelea kama jeshi au kitengo cha serikali.

Wakati awamu ya kwanza ya sitisho la mapigano ikitarajiwa kumalizika katika kipindi cha wiki mbili, Rubio alimwambia Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wakati aliposimama mjini Jerusalem kwamba kama Hamas inasimama kama kikosi ambacho kinaweza kutawala, au kama kikosi kinachoweza kusimamia au kama kikundi ambacho kinaweza kuwa tishio kwa matumizi ya ghasia, amani kupatikana itakuwa vigumu.

Forum

XS
SM
MD
LG