Shakira kupitia taarifa kwenye akaunti zake za Instagram na X Jumapili adhuhuri alisema kuwa sasa hivi yupo hospitalini na kwamba madaktari wake walisema hali yake haimruhusu kuimba."Nasikitika sana kwamba siwezi kuimba leo. Nilikuwa nimetazamia kwa hamu kuungana na mashabiki wangu wa Peru,” Shakira alisema. Nyota huyo aliwasili Peru Ijumaa jioni ambako alipangiwa kufanya show zake Jumapili na Jumatatu.
Peru ni taifa la pili kutembelea kwenye tour yake ya Latin Amerika baada kuwa Brazil kwa siku mbili wiki iliyopita. Mashabiki wake walimkaribisha kwa njia kubwa wakati wakimiminika kwenye viwanja vya ndege ili kumsalimia. “Asanteni sana kwa ukaribisho wenu hapa Lima," Shakira aliandika Jumamosi kupitia Instagram. Kupitia taarifa, Shakira alisema kuwa anatumai kupata nafuu hivi karibuni. “Matumaini yangu ni kufanya show zangu haraka iwezekanavyo. Timu yangu pamoja na promoter wanajitahidi kutafuta tarehe mpya, aliongeza kusema.
Forum