Shambulio la wanamgambo katika kambi ya jeshi limewaua wanajeshi sita kaskazini mwa Benin ambako wanajeshi wa serikali wanajaribu kuzuia mashambulizi ya mpakani yanayofanywa na makundi yenye silaha yenye itikadi kali ya Ki-Islam, msemaji wa jeshi amesema.
Shambulizi lisilotarajiwa la Jumamosi pia limesababisha vifo vya wanamgambo 17, msemaji Ebenezer Honfoga aliliambia shirika la habari la Reuters Jumapili jioni bila kutoa maelezo zaidi. Shambulio hilo linafuatia mauaji ya darzeni ya wanajeshi katika shambulio la mwezi Januari katika eneo la kaskazini la Alibori, ambalo lina Niger na Burkina Faso na limegubikwa na uasi.
Benin na Jirani yake wa pwani nchi ya Togo zote zinaathiriwa na mashambulizi katika miaka ya hivi karibuni wakati makundi yanayohusishwa na kundi la Islamic State na al-Qaeda yakipanua uwepo wao zaidi katika eneo la Sahel la Afrika Magharibi upande wa kaskazini.
Forum