Besigye, 68, ni mpinzani mkuu wa Rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni, aliye madarakani kwa takriban miaka 40 ambaye amempinga bila mafanikio katika chaguzi nne.
Katika kesi ya kutishia usalama wa taifa, Besigye aligoma kula kuanzia Februari 10 akipinga kuzuiliwa kwake, huku wakili wake akimuelezea kuwa mgonjwa sana.
“Hajakula, anakunywa maji tu,” mke wa Besigye, ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa UNAIDS, Winnie Byanyima, ameiambia AFP, Jumapili kando ya mkutano wa Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa.
Wakati Besigye alipoonekana hadharani mara ya mwisho, alipofikishwa mahakamani Ijumaa, alionekana akiwa dhaifu.
Forum