Mashambulizi makubwa yalifanyika karibu na kituo cha vifaa kilicho hatarini cha Pokrovsk, Kyiv imesema, huku maafisa wa Marekani na Russia, wakitarajiwa kufanya mazungumzo katika siku zijazo nchini Saudi Arabia na Rais wa Marekani, Donald Trump akishinikiza amani.
Jeshi la Kyiv limeripoti mapigano 261 na Russia, katika saa 24 siku ya Jumamosi, ikiwa ni idadi kubwa zaidi iliyorekodiwa mwaka huu na zaidi ya mara mbili ya takriban 100 kwa siku kuliko ilivyoripotiwa siku zilizopita.
βLeo ilikuwa siku ngumu zaidi ya 2025 kwenye uwanja wa mapambano,β blogu ya kijeshi ya Ukraine, ya DeepState iliandika Jumamosi jioni.
Forum