“Ni lazima niseme kwamba iwapo Syria itaendelea na ukuaji wa miaka mitano iliyopita wa asilimia 1.3 ya mapato ya ndani kila mwaka, itachukua miaka 55 kururejea kwenye viwango vya 2010,” alisema naibu msimamizi wa UNDP, na pia mratibu wa ofisi ya kieneo ya mataifa ya Kiarabu iliyotoa ripoti hiyo, Abdallah Al Dardar.
Al Dardari wakati akizungumza na wanahabari akiwa Nairobi alisema kuwa mauaji ya zaidi ya Wasyria 600,000, kupotezwa kwa wengine 113,000 , uharibifu mkubwa wa mali na kupoteza dhamani ya sarafu, uhaba wa fedha za kigeni, ukosefu wa ajira na asilimia 90 ya watu wakiwa kwenye hali ya umasikini, vinachangia mazingira magumu ya kurejea kwenye hali ya kawaida.
Kulingana na ripoti hiyo, mwaka uliyotanguliwa kuzuka kwa mapigano, mapato ya ndani ya Syria yalikuwa dola bilioni 62 kwa mwaka, na ilikuwa na ukuaji wa zaidi ya asilimia 5 ndani ya miaka mitano iliyotangulia.
Forum