Hatua hiyo inafuatia tangazo la mwendesha mkuu wa mashtaka wa ICC, mwezi uliopita, la kutaka kiongozi wa juu zaidi wa Taliban Hibatullah Akhundzada na washirika wake wa karibu kukamatwa.
ICC inawashutumu kwa kuwajibika na uhalifu wa kuwatesa wanawake na wasichana wa Afghanistan.
Taliban walichukua uongozi wa Afghanistan mnamo Agosti 2021, kutoka kwa serikali iliyokuwa ikitambuliwa kimataifa ya Kabul, iliyoanguka baada ya Marekani kuondoa wanajeshi wake nchini humo baada kulinda amani kwa muda wa miongo miwili.
Taliban, wanaongoza Afghanstan kwa kutumia sheria kali za Kiislamu, na kuwawekea vizuizi vikali wanawake ikiwemo kukandamiza uhuru wa kujieleza, kuwazuia kusoma shuleni na kushiriki shughuli za uma katika jamii.
Hakuna nchi imetambua utawala wa Taliban kutokana na namna wamewakandamiza wanawake na Watoto wasichana.
Forum