Tangazo hilo sasa linabatilisha hatua ya utawala wa Biden mwaka jana ya kuongeza muda wa program hiyo hadi Februari 2026, msemaji huyo amesema, akiongeza kuwa hatua hiyo haikuwa muhimu. Rais Donald Trump ambaye ni Mrepablikan wakati wa muhula wake wa kwanza kati ya 2017- 2021 alijaribu kumaliza program hiyo ambayo pia inajulikana kama TPS, lakini alizuiliwa na mahakama za serikali kuu.
Mapema mwezi huu Noem alifuta program hiyo kwa raia 600,000 wa Venezuela, wakati nusu yao wakipoteza vibali vya kufanya kazi. Zaidi ya watu milioni 1 zaidi ya nusu wakiwa watoto wamekosehwa makazi ndani ya Haiti ambako ghasia za magenge zimeshamiri licha ya juhudi za Umoja wa Mataifa za kutumia walinda usalama mwaka uliopita, data za Umoja huo zilizochapishwa Januari zinaonyesha. Tangu 2023, Haiti haijakuwa na viongozi wa kuchaguliwa na wala haijafanya uchaguzi tangu 2016.
Forum