Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 02, 2025 Local time: 15:49

Trump anataka Marekani kumiliki Gaza

Rais wa Marekani Donald Trump
Rais wa Marekani Donald Trump

Rais wa Marekani Donald Trump amesema anataka Marekani kuchukua umiliki wa Gaza, hatua inayovuka matamshi yake ya kuwalazimisha wapalestina kuondoka katika eneo eneo lililokumbwa na mapigano na kuhamia nchi jirani za Jordan na Misri.

Trump amesema hayo wakati wa kikao na waandishi wa habari huko White House, akiwa na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, jana Jumanne jioni.

Katika siku za hivi karibuni, maelfu ya wapalestina katika maeneo ya kusini mwa Gaza wamekuwa wakielekea kwenye makazi yao baada ya Israel kuwaruhusu kurudi huko kama sehemu ya makubaliano ya sitisho la mapigano na kuachiliwa kwa mateka wanaoshikiliwa na Hamas.

Trump amesema anataka kuliendeleza eneo hilo na kuwa kile alichokiita Mandhari ya Mashariki ya Kati.

Netanyahu amesema kwamba moja ya malengo yake ya vita ni kuhakikisha kuwa Hamas sio tishio tena kwa Israel lakini akasema Trump analichukua hilo katika hatua ya ngazi ya juu zaidi.

Trump hata hivyo hajatoa maelezo namna anavyopanga kudhibithi Gaza iliyoharibiwa na vita vya takriban miezi 15.

Forum

XS
SM
MD
LG