Ramaphosa anatarajiwa kulihutubia taifa kesho Alhamisi kuhusu utendakazi wa serikali hiyo, kwa mara ya kwanza tangu ilipoundwa.
Kumekuwepo na mizozo kadhaa ndani ya serikali kuhusu mpango wa kufundisha lugha ngeni shuleni na uhusiano mzuri kati ya Ramaphosa na utawala wa Russia, ambavyo vimetishia kuisambaratisha serikali yake.
Mzozo umetokea pia baada ya Ramaphosa kusaini sheria inayoiruhusu serikali kumiliki mashamba kutoka kwa watu binafsi kwa maslahi ya umma, bila kulipa fidia, lakini amefutilia mbali madai ya kuwepo mpasuko ndani ya serikali yake akisema yanayoelezwa sio sahihi na kwamba viongozi ndani ya serikali huwa wanafanya mazungumzo.
Forum