Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 02, 2025 Local time: 17:48

Ghasia za magenge zasababisha mauaji Equador


Picha ya maktaba ya polisi wa kupambana na magenge.
Picha ya maktaba ya polisi wa kupambana na magenge.

Ghasia kati ya makundi hasimu ya magenge zimeua watu 14 mwishoni mwa wiki kwenye mji wa bandari wa Equador wa Guayaquil ambao ni kitovu cha mivutano kati ya magenge, polisi wamesema Jumatatu.

Kwenye kisa kimoja, watu waliyokuwa kwenye pikipiki walimiminia watu risasi nje ya duka moja na kuua mtoto pamoja na watu wazima 6, mkuu wa polisi Santiago Tuston, amesema, akihofia mashambulizi ya kulipiza kisasi.

Video zilizowekwa kwenye mitandao ya kijamii zimeonyesha miili ikiwa imetapakaa kwenye barabara kaskazini mwa mji wa Guayaquil. Tuston alisema kuwa maujai hayo ambayo nia yake haijabainishwa yamefikisha jumla ya watu 14 mwishoni mwa wiki kwenye mji wa Guayaquil.

Guayaquil ni mjii mkuu wa jimbo la kusini magharibi la Guayas ambapo hali ya dharura imekuwepo tangu Januari wakati mamlaka zikijitahidi kukabiliana na ghasia kwenye taifa hilo la kusini mwa Amerika ambalo kwa muda mrefu limekuwa na amani.

Equador ni nyumbani kwa takriban makundi 20 ya magenge yanayohusika kwenye ulanguzi wa dawa za kulevya, utekaji nyara, na uitishaji wa fidia likiwa taifa la watu milioni 18 likiwa kati ya mataifa makubwa yenye kuzalisha dawa aina ya cocaine ya Peru na Colombia.

Katika miaka ya karibuni, taifa hilo limegubikwa na ghasia za magenge na hasa kwenye kwenye mji wa bandari wa Guayaquil unaotumiwa kutuma dawa za kulevya Marekani na Ulaya.

Forum

XS
SM
MD
LG