Takriban wanajeshi 15 wa Puntland na zaidi ya wanamgambo 50 walikufa kwenye mapigano hayo kwenye maeneo ya Dharin na Qurac kwenye milima ya Cal Miskaad huko Bari Puntland. Taarifa hizo zimetolewa na maafisa kadhaa wa usalama wa Puntland wakizungumza na VOA kwa masharti ya kutotambulishwa kwa kuwa hawajaruhusiwa kuongea na vyombo vya habari.
Kwenye mahojiano ya Jumatano na VOA Idhaa ya Kisomali, msemaji wa operesheni ya usalama wa Puntland Brigedia Jenerali Mohamud Ahmed alisema kuwa mapigano hayo yaliyoanza Jumanne yalikuwa mabaya zaidi tangu Puntland ilipoanza mashambulizi mwezi uliyopita dhidi wanamgambo wa Islamic State ambao wana mahandaki kwenye sehemu za milima.
“Tumedhibitisha kuwa takriban wanamgambo 57 wa Islamic State wote wakiwa raia wa kigeni waliuwawa kwenye mapigano katika saa 24 zilizopita,” Ahmed alisema. Hata hivyo Ahmed hakusema ni wanajeshi wangapi wa Puntland waliuwawa au kujeruhiwa ingawa aliashiria kuwa idadi ilikuwa kubwa.
Forum