Muda kati ya kuanza kwa dalili na kifo ni saa 48, kwa idadi kubwa ya visa, na “hicho ndicho kinachotia wasi wasi mkubwa,” Serge Ngalebato mkurugenzi wa huduma za afya katika hospitali ya Bikoro ameliambia shirika la Habari la Associated Press.
Mlipuko huo wa hivi karibuni huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umeanza Januari 21 na visa 419 vimerikodiwa vikiwemo vifo 53.
Kulingana na ofisi ya WHO Afrika, mlipuko wa kwanza ulitokea katika mji wa Boloko baada ya watoto watatu kula popo na kufa katika kipindi cha saa 48 baada ya kupata homa kali.
Forum