Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 20, 2025 Local time: 23:58

Waandishi wakabiliana na habari potofu kuhusu afya na matibabu mjini Goma


Vita vya Afrika Dhidi ya Taarifa Potofu na za Upotoshaji
Vita vya Afrika Dhidi ya Taarifa Potofu na za Upotoshaji

Katika mji wa Goma, kundi la waandishi wa habari wa Congo wanakabiliana na habari potofu chungu nzima kuhusu afya na matibabu, ambazo ni hatari kubwa sana kwa umma.

Waandishi hawa wa habari wanaofanya kazi mjini Goma. Wanapambana na habari za uongo kuhusu vita na magonjwa.

Jarida la Eleza Ukweli

Katika eneo linalopambana na changamoto za afya na kukumbwa na vita, waandishi wa kubaini habari za uongo katika jarida la Eleza ukweli, wanatafuta habari za ukweli kuhusu fikra zinazoambatana na ugonjwa mpox ambao awali ulikuwa unajulikana kama ugonjwa kutoka kwa nyani. Habari za uongo zinasema kwamba ugonjwa huo haupo kabisa na kwamba yanayosemwa ni upele tu ambao hauna madhara.

Aline Kataliko anasema kazi yao ni muhimu sana kwa afya ya umma na katika kujenga imani katika jamii.

Aline Kataliko wa Eleza Fact: 'Kuna uvumi kuhusu mpox, unaosema kwamba lengo la chanjo ni kuondoa kizazi cha raia wa Congo. Tunaangazia hatari za uvumi huo na namna unavyoweza kuathiri jamii yote kwa jumla na kuzuia juhudi za kumaliza maambukizi."

Habari Potofu

Tangu mwaka 2021, waandishi wa habari 25 katika jarida la Eleza ukweli, akiwemo Joel Alimasi Kitambala, wamekuwa wakiangazia na kueneza habari kuhusu hatari za habari potofu. Joel Alimasi Kitambala ni mwandishi wa habari katika Eleza Ukweli.

Joel Alimasi Kitambala wa Eleza Fact: Kutambua ukweli, tunatumia maneno muhimu na kila wakati kuna chapisho ambalo lina maneno hayo, tunapata taarifa kuhusu chapisho hilo. Kama kuna hja ya kuchambua jarida hilo, waandishi wa kutafuta ukweli wanapewa jukumu wanaolifanyia kazi.

Makala yanayochapishwa na Eleza ukweli, yanachapishwa kwenye wavuti, na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii na kutangazwa kwenye vituo vya radio ili kuwafikia wale wasiotumia internet.

Taarifa za Uongo juu ya Afya na Tiba

Kuna taarifa nyingi za uongo kuhusu afya na tiba kama taarifa zilizotolewa kuhusu mpox. Mwandishi wa habari Joylen Kazimoto aliripoti kuhusu habari potofu kuhusu virusi vya Corona kwa kutumia njia ya internet - podcast. Joylen Kazimoto ni mwandishi wa Eleza ukweli.

Raia kupambana na Virusi vya Corona

Joylen Kazimoto wa Eleza Fact anaeleza: "Mjini Kinshasa, ninapoishi, nimegundua kwamba kuna hali ya kutojali kuhusu raia kupambana na virusi vya Corona kwa sababu watu wengi hawaamini kwamba kuna ugonjwa huo. idadi kubwa ya watu wasioamini kwamba kuna ugonjwa ni wale wanaoishi nje ya mji."

Daniel Makeke ni mhariri. Anasema juhudi hizo ni muhimu katika kupambana na habari potofu.

Anaeleza kuwa: "Vituo vya radio vinategemea podcasts ili kueneza taarifa kuhusu magonjwa na majanga, namna ya kupata tiba, ukweli kuhusu tiba na chanzo cha monkeypox, miongoni mwa mengine. Kwa namna hiyo, tunaweza hata kuwafikia watu wasiokuwa na uwezo wa mtandao wa kidijitali ambao wanafaidika na kazi yetu ya kutafuta ukweli."

Makeke anasema juhudi za Eleza ukweli zinasaidia kuzuia kusambaa kwa habari za uongo kuhusu magonjwa kusambaa, zinazoweza kuwa hatari kwa afya.

((Zanem Nety Zaidi, VOA Africa, Goma, Democratic Republic of Congo.))

Forum

XS
SM
MD
LG