Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 14:05

Majimbo kadhaa yataka mtandao wa X kurekebisha taarifa potofu za uchaguzi


Mmiliki wa mtandao wa X, Elon Musk
Mmiliki wa mtandao wa X, Elon Musk

Makatibu watano wa majimbo ya Marekani wanamsihi mmiliki wa mtando wa X, Elon Musk kurekebisha program ya Akili Mnemba ya “chatbot” kwenye mtandao wa X, wakisema katika barua iliyotumwa Jumatatu kwamba imeeneza habari potofu za uchaguzi.

Maafisa wakuu wa uchaguzi kutoka Michigan, Minnesota, New Mexico, Pennsylvania na Washington walimwambia Musk kwamba “chatbot,” ya X “Grok,” ilitoa taarifa za uongo kuhusu tarehe za mwisho za kura za jimbo muda mfupi baada ya Rais Joe Biden, kujiondoa katika kinyang’anyiro cha urais wa 2024.

Ingawa “Grok,” inapatikana tu kwa watumiaji waliojisajili kwa matoleo ya kwanza ya X, habari potofu ilishirikiwa kwenye majukwaa mengi ya mitandao ya kijamii na kufikia mamilioni ya watu, kwa mujibu wa barua hiyo.

Forum

XS
SM
MD
LG