Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 20, 2024 Local time: 01:57

Russia: Google yalipishwa faini ya dola za Marekani 32,000 kwa kilichodaiwa kutofuta habari potofu


FILE PHOTO: Nembo ya Kampuni ya Google
FILE PHOTO: Nembo ya Kampuni ya Google

Mahakama moja nchini Russia Alhamisi ilitoa adhabu kwa kampuni ya Google kulipa faini ya dola za Marekani 32,000 kwa kushindwa kufuta kile kilichodaiwa ni taarifa potofu kuhusu vita vya Ukraine.

Hatua hiyo ya mahakama ya Hakimu mkazi hiyo inafuatia hatua kama hivyo iliyochukuliwa mapema mwezi Agosti dhidi Taasisi ya Wikimedia ambayo inaendesha Wikipedia.

Kulingana na taarifa za habari za Russia, mahakama hiyo iligundua kuwa huduma za kanda za video za Youtube, ambazo zinamilikiwa na Google, zilikuwa na hatia ya kutofuta kanda za video zilizokuwa na taarifa potofu kuhusu vita hivyo – ambayo Russia inaielezea kuwa “ni operesheni maalum ya kijeshi.”

Google pia ilikutwa na makosa ya kutoondoa video kadhaa ambazo zilikuwa zinapendekeza namna ya kufanikisha kuingia katika majengo ambayo hayaruhusu watoto kuingia, mashirika ya habari yalisema, bila ya kufafanua ni aina gani ya majengo yaliyohusika.

Nchini Russia, mahakama ya hakimu mkazi kawaida inashughulikia uvunjaji wa sheria za kiuongozi na kesi za uhalifu wa ngazi ya chini.

Tangu ilipopeleka majeshi yake nchini Ukraine mwezi Februari 2022, Russia imepitisha hatua kadhaa za adhabu dhidi ya ukosoaji au kuhoji juu ya kampeni yake ya kijeshi.

Baadhi ya wakosoaji wamepewa adhabu kali. Kiongozi wa Upinzani Vladimir Kara-Murza alihukumiwa mwaka huu kifungo cha miaka 25 jela kwa uhaini kutokana na hotuba zake alizotoa dhidi ya hatua ya Russia nchini Ukraine.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP.

Forum

XS
SM
MD
LG