Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 05:31

Google, Microsoft zaishutumu sheria inayopinga ushoga Uganda


Nembo ya Google inaonekana ikiwa na bendera ya upinde wa mvua kama ishara ya wasagaji, mashoga, wapenzi wa jinsia mbili, waliobadili jinsia (LGBT) , tarehe 7 Juni 2022. Picha na Angela Weiss / AFP.
Nembo ya Google inaonekana ikiwa na bendera ya upinde wa mvua kama ishara ya wasagaji, mashoga, wapenzi wa jinsia mbili, waliobadili jinsia (LGBT) , tarehe 7 Juni 2022. Picha na Angela Weiss / AFP.

Muungano wa makampuni ya kimataifa, yakiwemo Google na Microsoft, Jumatano yameushutumu mswaada uliopitishwa na bunge la Uganda wiki iliyopita dhidi ya ushoga na kuionya kuwa sheria hiyo itakuwa na athari za kiuchumi kwa nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Muungano wa makampuni ya biashara yamesema sheria hii, ambayo inaharamisha watu kujitambulisha kama wasagaji, mashoga, watu wa jinsia mbili au waliobadili jinsia itazuia mtiririko wa uwekezaji na watalii nchini humo.

Mswaada huo unaweka adhabu ya kifo kwa wale watakao tenda vitendo vya ushoga uliokithiri, mswaada huo pia umefafanua kuwajumuisha wale watakao jihusisha na mahusiano ya mapenzi ya jinsia moja na watoto wenye umri

chini ya miaka 18 au wakati mhusika ana Virusi Vya Ukimwi, miongoni mwa makundi mengine.

Mswaada huo ambao umepitishwa na bunge, unasubiri kutiwa saini na rais Yoweri Museveni ili kuwa sheria.

White House ilisema wiki iliyopita mswaada huo unatia wasi wasi na kwamba ni miongoni mwa hatua kali sana zilizochukuliwa dhidi ya jumuiya ya mashoga duniani.

Museveni bado hajatoa maoni yake kuhusiana na mswaada huo, ingawa aliwahi kutia saini sheria kama hiyo mwaka 2014 ambayo ilizua tuhuma za kimataifa kabla ya kubatilishwa na mahakama ya ndani ikidai sheria hiyo haikufuata taratibu za kimsingi.

Pia waziri wa habari wa Uganda Chris Baryomunsi hakuweza kupatikana mara moja kutoa maoni.Miongoni mwa wanachama wa muungano huo wa Open for Business, ni Google, Mastercard Unilever, Standard Chartered, PwC na Deloitte ambayo yanafanya operesheni zake nchini Uganda.

XS
SM
MD
LG