Ndawula mwenye umri wa miaka 26, alisema mwenye nyumba wake alimuonyesha video hiyo iliyowekwa kwenye mtandao na mtu asiyejulikana, na kisha kumpa notisi ya kumfukuza kwenye nyumba akisema kuwa nyumba yake haipangishwi kwa mtu ambaye ni shoga.
“Mimi sasa nimekuwa tishio kwa watoto wanaonizunguka kwa sababu wataniiga na kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja,” kwa utani Ndawula aliliambia shirika la habari la Reuters.
Anayoyapitia Ndawula ni moja ya matukio ya wimbi la ubaguzi na unyanyasaji dhidi ya wasagaji, mashoga , watu wa jinsia mbili na wale waliobadili jinsia. Ubaguzi ulioanza tangu bunge lilipotangaza uchunguzi wake, wanaharakati wanasema.
Zogo limezidi kuathiri jamii ya LGBT ambayo tayari iko hatarini nchini Uganda, ambako watu wenye mahusiano ya jinsia moja hupewa adhabu ya kifungo cha maisha jela.
Waziri wa habari Chris Baryomunsi hakujibu maswali kuhusu athari za uchunguzi huo. Cuthbert Abigaba, mbunge anayeongoza uchunguzi huo, aliiambia Reuters kuwa "hasumbuliwi na chochote kinachosemwa na watu wa wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.
Chanzo cha habari ni shirika la habari la Reuters