Serikali ya Uganda imesitisha shughuli za shirika lisilo la kiserikali la nchini humo linalotetea haki za kingono za walio wachache likilishutumu kwa kufanya kazi katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki kinyume cha sheria, kwa mujibu wa afisa mwandamizi.
Shirika hilo nchini Uganda (SMUG) kwa miaka mingi limekuwa likipigia debe haki za wapenzi wa jinsia moja nchini Uganda, ambako mapenzi ya jinsia moja bado ni kinyume cha sheria na watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja wanakabiliwa na kukamatwa, kutengwa na vurugu.
Operesheni za SMUG zimesitishwa kwa sababu zilikuwa zikifanya kazi kinyume cha sheria, Stephen Okello, ambaye anaongoza idar aya serikali inayosimamia mashirika yasiyo ya kiserikali, alisema katika taarifa iliyopewa Reuters siku ya Jumamosi.
SMUG inaendelea kufanya kazi bila kibali halali alisema na kuongeza kuwa shughuli za shirika hilo zimesitishwa mara moja.
Shirika la SMUG kwa miaka mingi limekuwa likitetea haki za watu wa mapenzi ya jinsia moja nchini Uganda, ambapo ushoga bado ni haramu na mashoga wanakabiliwa na kukamatwa, kutengwa na ghasia.