Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:16

Ushoga unakiuka maadili - Museveni


Watu wakiwa wamevaa vinyago kwenye maandamano ya kwanza ya kujivunia mashoga nchini Uganda, Agosti 9, 2014. Picha na ISAAC KASAMANI / AFP.
Watu wakiwa wamevaa vinyago kwenye maandamano ya kwanza ya kujivunia mashoga nchini Uganda, Agosti 9, 2014. Picha na ISAAC KASAMANI / AFP.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni siku ya Alhamisi aliwaelezea mashoga kuwa ni "wapotovu" na kutaka uchunguzi ufanywe kuhusu ushoga huku wabunge katika taifa hilo lla Afrika Mashariki wakijiandaa kuupigia kura mswaada dhidi ya LGBT.

Mswaada huo uliowasilishwa mapema mwezi huu, unapendekeza adhabu kali kwa watu wenye uhusiano wa kimapenzi wa jinsia moja katika nchi ambayo ushoga tayari ni kinyume cha sheria, na kusababisha ukosoaji kutoka kwa mashirika ya kutetea haki za binadamu.

Akihutubia kuhusu hali ya kitaifa mbele ya bunge, Museveni, ambaye ametawala Uganda tangu 1986, amewataja mashoga kuwa watu wapotovu wakati wabunge wakimtaka atoe maoni yake kuhusu sheria hiyo mpya.
"Ushoga ni mwenendo wa tabia unaokiuka maadili. Kwa nini? Je hii ni asili yetu au inatokana na malezi. Tunahitajika kujibu maswali haya," kiongozi huyo wa miaka 78 alisema.

Kwa mujibu wa sheria iliyopendekezwa, mtu yeyote anayejihusisha na mapenzi ya jinsia moja au anayejitambulisha kama LGBTQ anaweza kukabiliwa na kifungo cha hadi miaka 10 jela.

Mswaada huo umekuja wakati nadharia za njama zikishutumu mashirika ya kimataifa kuhamasisha ushoga kupata umaarufu kupitia mitandao ya kijamii nchini Uganda.

"Nchi za Magharibi zinapaswa kuacha kupoteza muda wa watu kwa kujaribu kulazimisha mila zao kwa watu wengine," Museveni alisema katika hotuba iliyosusiwa na wabunge wote wa upinzani isipokuwa mbunge mmoja.

Mswaada huo unatarajiwa kujadiliwa wiki ijayo, na kura huenda ikapigwa Jumanne asubuhi.

Lakini tangu nchi hiyo ipate uhuru kutoka kwa Uingereza mwaka 1962 haijawahi kumtia hatiani mtu yeyote aliyetumuhiwa kufanya mapenzi ya jinsia moja.

Mwaka 2014 wabunge wa Uganda ilipitisha mswaada uliotaka kifungo cha maisha jela kwa watu watakaopatikana na hatia ya kufanya mapenzi ya jinsia moja.

Mahakama baadaye ilitupilia mbali sheria hiyo kutokana na mapungufu ya kiufundi, Lakini sheria hiyo ilikuwa tayari imezua shutuma kimataifa, baadhi ya mataifa ya Magharibi yalizuia au kusimamisha upelekaji wa misaada ya mamilioni ya dola kwa serikali ya Uganda.

Wafuasi wa LGTB nchini Kenya. Picha na shirika la habari la AP Photo/Ben Curtis, Maktaba.
Wafuasi wa LGTB nchini Kenya. Picha na shirika la habari la AP Photo/Ben Curtis, Maktaba.

Huko nchini Kenya mpiga gitaa Arnold alijitokeza kama shoga miaka kadhaa iliyopita, lakini mwezi uliopita, mpiga gitaa huyo aliondoa bendera ya upinde wa mvua kwenye wasifu wake wa Twitter, akihofia usalama wake wakati wimbi jipya la chuki dhidi ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja kuenea huko Afrika Mashariki.

Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 35, ambaye aliomba jina lake halisi lisitajwe, aliliambia Shirika la habari la AFP kuwa ana wasiwasi serikali inaweza kutumia mitandao ya kijamii kuwatambua na kuwakamata watu walio katika jamii ya LGBTQ.

"Maeneo salama yanapungua kila siku," alisema. "Si muda mrefu , hatutakuwa na mahala pa kujificha,” alisema Arnold

Kenya, kama majirani zake , inakabiliana na mzozo mkubwa wa gharama ya maisha na imekuwa ikikabiliwa na ukame mbaya sana kuwahi kutokea kwa kipindi cha miongo minne.

Lakini wanaharakati wanasema matatizo hayo yamewekwa kando wakati viongozi kote katika wigo wa kisiasa wakiungana kuanzisha kampeni " inayofadhiliwa na serikali dhidi ya ubaguzi wa watu wenye mahusiano ya jinsia moja ".

Nchini Kenya na Tanzania, mapenzi ya jinsia moja bado ni uhalifu chini ya sheria iliyokuwa imewekwa wakati wa utawala wa ukoloni na adhabu inajumuisha kifungo cha hadi miaka 14 jela.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP.

XS
SM
MD
LG