Sheria hyo imekuwa ikitumika kulind makampuni hayo dhidi ya kushitakiwa kutokana na taarifa zinazorushwa kupitia majukwaa yake. Majaji wa mahakama hiyo wamesikiliza hoja ya iwapo familia ya kimarekani ya mwanafunzi wa chuo aliyeuwawa kwenye shambulizi la kigaidi mjini Paris, inaweza kushitaki Google kwa kusaidia magaidi kueneza ujumbe wao na kuvutia vijana wapya kujiunga nao.
Hiyo ndiyo kesi ya kwanza inayomulika sheria ya maadili ya mawasiliano nambari 230, iliyopitishwa 1996, kwa nia ya kulinda makampuni dhidi ya mashitaka kutokana na taarifa zinazowekwa kwenye mitandao yao. Mahakama za chini zimetetea sheria hiyo zikisema kwamba inalinda sekta ya internet, huku makampuni ya mawasiliano pamoja na washirika wao wakisema kwamba imechochea ukuaji wa Internet pamoja na kudhibiti ujumbe hatari kuwekwa kwenye mitandao.