Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 12:20

TikTok kupambana na habari potofu zinazolenga uchaguzi ujao wa EU


FILE - The icon for the video-sharing TikTok app is seen on a smartphone, Feb. 28, 2023, in Marple Township, Pa. The Biden '24 presidential campaign is using TikTok despite security concerns about it.
FILE - The icon for the video-sharing TikTok app is seen on a smartphone, Feb. 28, 2023, in Marple Township, Pa. The Biden '24 presidential campaign is using TikTok despite security concerns about it.

TikTok inachukua hatua kukabiliana na habari potofu kuhusu uchaguzi ujao wa Umoja wa Ulaya, ikiwa ni pamoja na kuweka vituo vya kuhakiki taarifa ndani ya programu ya app yake, jukwaa hilo ambalo husambaza kanda za video lilisema Jumatano katika makala iliyochapishwa katika blogi yake.

TikTok inapanga kuzindua app ya lugha mbali mbali ya “vituo vya uchaguzi” vya Umoja wa Ulaya, EU, hapo mwezi ujao katika nchi zote 27 za Umoja huo ili kwamba “watu waweze kutofautisha ukweli kutokana na uongo.”

Mamilioni kadhaa ya wazungu wanatarajiwa kupiga kura mwezi Juni kuchagua wabunge 720 wa bunge la umoja huo katika uchaguzi unaofanyika mara moja kila baada ya miaka mitano.

Wakati nchi zaidi ya 50 zikijiandaa kufanya uchaguzi wa kitaifa mwaka 2024, kampuni za teknolojia zinafanya juhudi mbalimbali kuepusha majaribio ya kuvuruga uchaguzi, ikiwemo kupitia matumizi ya program ya komputa, Artificial Intelligence, AI kuharakisha usambaaji wa habari za kupotosha au utengenezaji wa picha au video zenye kupotosha.

TikTok, ambayo ina wafanyakazi 6,000 wanaosimamia udhibiti wa maudhui zilizopo katika lugha za EU, iliashiria kuwa inajitayarisha kukabiliana na taarifa potofu zaidi, operesheni za ushawishi za kisiri na taarifa potofu zinazotolewa na AI wakati wa kipindi cha uchaguzi.

TikTok ilisema kanda za video zinazo husiana na uchaguzi wa EU zitawekewa alama ili kuwaelekeza watu kuingia katika app za kituo cha uchaguzi cha nchi zao.

Vituo hivi vitaweza, kwa msaada wa tume za uchaguzi za kila nchi na makundi ya jumuiya za kiraia, kutoa “taarifa za kuaminika na rasmi” kuhusu kupiga kura, alisema mkuu wa usalama na ukweli wa TikTok, Kevin Morgan.

Vituo hivyo vya uchaguzi vya EU viliundwa kwa shughuli sawa na hiyo kwa ajili ya uchaguzi wa kitaifa wa hivi karibuni huko Ugiriki, Uholanzi, Poland, Slovakia na Uhispania.

TikTok, inayomilikiwa na kampuni ya ByteDance ya China, inawateja milioni 134 wa Ulaya. Morgan alisema maafisa wengi wa Ulaya wako katika jukwaa hilo, ikiwa ni pamoja na kiasi cha theluthi ya wabunge wa EU.

Kampuni hiyo pia itaweka “ofisi ya udhibiti” maalum kwa ajili ya uchaguzi katika makao makuu ya Ulaya iliyoko Dublin ikiwa na wataalam kutoka kitengo chake cha uaminifu na usalama.

Forum

XS
SM
MD
LG