Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 08:43

Somali yaamuru mitandao ya kijamii ya Tik Tok na Telegram ifungwe


Tik Tok
Tik Tok

Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Somalia imeagiza mamlaka inayoratibu utoaji wa  huduma za intaneti nchini humo kuzima uwezo wa kufikia mitandao ya kijamii ya  TikTok, Telegram, na tovuti ya kamari ya 1xBet.

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia, Jama Hassan Khalif, alitoa agizo hilo katika taarifa yake ya Jumapili, akitaja sababu za kuzuia makampuni hayo kuwa ni usalama na kupambana na ugaidi.

Taarifa hiyo ilisema ukiukaji wa mara kwa mara sheria wa makundi ya kigaidi yanayotumia mitandao ya kijamii huathiri usalama na utulivu wa jamii.

Wizara hiyo ilisema inafanya kazi kulinda maadili ya watu wa Somalia wakati wa kutumia njia za mawasiliano ya mtandaoni ambazo ilisema zimeathiri mfumo wa maisha na kuongeza kile ilichosema ni "tabia mbaya," kulingana na taarifa hiyo.

"Unaamriwa kuzima mitandao iliyotajwa hapo juu kufikia Alhamisi Agosti 24, 2023 saa kumi na moja jioni," Khalif alisema katika taarifa hiyo.

"Yeyote ambaye hatafuata agizo hili atakabiliwa na hatua za kisheria zilizo wazi na zinazofaa," aliongeza.

Kundi la wanamgambo wa al-Shabab mara kwa mara hutumia huduma ya kutuma ujumbe ya Telegram ili kuchapisha video zake, taarifa kwa vyombo vya habari, na sauti za mahojiano na makamanda wao.

Al-Shabab mara nyingi huchapisha habari kuhusu mashambulizi yake kwenye Telegram na tovuti nyinginezo, ndani ya dakika chache, baada ya kutokea. Kikundi hicho huunda akaunti mpya mara kwa mara pindi tu akaunti zao za Telegram zinapofungwa.

TikTok inaaminika kuwa tovuti inayokua kwa kasi zaidi nchini Somalia, na inatumiwa na vijana na hata viongozi wa serikali.

Forum

XS
SM
MD
LG