Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 31, 2025 Local time: 04:13

Ukraine na Marekani zakaribia kufikia makubaliano kuhusu madini ya Ukraine


Rais wa Marekani Donald Trump na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy. Picha ya Reuters
Rais wa Marekani Donald Trump na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy. Picha ya Reuters

Marekani na Ukraine Jumapili zimesema zinakaribia kufikia makubaliano kwa Kyiv Kuipa Washington Sehemu kubwa ya madini yake nadra kama malipo ya fidia kwa mabilioni ya dola ya zana za kijeshi ambazo Marekani iliipa Ukraine kujihami dhidi ya vita vya Russia.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy aliuambia mkutano wa waandishi wa habari mjini Kyiv kwamba Ukraine na Marekani “zimepiga hatua” ili kufikia makubaliano.

Alisema rasimu ya mkataba huo inaitaka Ukraine kulipa dola 2 za Marekani kwa kila dola ya msaada ambayo Marekani iliipa Kyiv kupambana na uvamizi wa Russia, ingawa maelezo ya makubaliano hayo bado hayajawekwa hadharani.

Marekani imekuwa mfadhili mkubwa wa Ukraine, kwa kuipa nchi hiyo msaada wa kijeshi na wa kibinadamu wa dola bilioni 128, kulingana na taasisi ya Ujerumani ya Kiel inayofuatilia masuala ya uchumi wa dunia.

Msaada wa Marekani ndio mkubwa ukilinganisha na msaada wa dola bilioni 124 kwa mataifa yote 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya.

Mjumbe maalum wa Marekani Steve Witkoff amekiambia kipindi cha televisheni ya CNN “State of the Union” kwamba anatarajia Zelenkiy atasaini mkataba kuhusu madini wiki hii.

Forum

XS
SM
MD
LG