Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 07, 2025 Local time: 08:46

Wanajeshi 18 wa Pakistan wauwawa


Serekali ya Pakistani, Jumamosi imesema kwamba wanajeshi wasiopungua 18 wameuwawa katika shambulizi la usiku wa kuamkia jana katika jimbo la Balochistan, likiashiria moja ya siku mbaya zaidi kwa vikosi vya usalama katika miezi ya hivi karibuni.

Taarifa ya jeshi imesema kuwa majeruhi hao walitokea katika wilaya ya Kalat, Ijumaa usiku, wakati magaidi walipojaribu kuweka vizuizi barabarani katika eneo hilo, na vikosi vya usalama vilijibu mara moja kile kilichoitwa kitendo cha uoga cha kigaidi.

Jeshi limesema takriban washambuliaji 12 waliuwawa katika mapigano yaliyofuata. Ofisi ya Waziri Mkuu wa Pakistani, Shehbaz Sharif, mjini Islamabad imesema katika taarifa yake kwamba amelaani vikali shambulizi hilo dhidi ya vikosi vya usalama.

Mfululizo wa oparesheni za usalama zimeanzishwa katika eneo lote la Balochistan toka usiku shambulizi lililouwa magaidi wasiopungua 11 na kuharibu maficho yao Jumamosi, kwa mujibu wa taarifa ya jeshi.

Forum

XS
SM
MD
LG