Mfumo wa ulinzi wa anga wa Ukraine umetungua na kuharibu ndege sizizokuwa na rubani 59 kati ya 102 zilizorushwa.
Jeshi la anga la Ukraine limesema ndege zisizokuwa na rubani 37 zilipotoshwa na mfumo wa elektroniki wa Ukraine na hivyo kutofikia malengo.
Mashambulizi ya ndege zisizokuwa na rubani za Russia yamesbabisha uharibifu katika mikoa ya kaskazini mashariki ya Sumy, odesa, sehemu za kusini nakatikati mwa mkoa wa Cherkasy.
Gavana wa Odesa Oleh Kiper, amesema raia wanne, akiwemo daktari wamejeruhiwa katika mashambulizi hayo yaliyolenga mji wa Chornomorsk.
Forum