Wizara ya ulinzi ya Russia, imesema wanajeshi wake walikiteka kijiji cha Krymske, katika vitongoji vya kaskazini mashariki vya Toretsk, iliyoko katikamkoa wa mashariki wa Donetsk, na eneo la mapigano makali katika miezi ya hivi karibuni. Jeshi la Russia, linasonga mbele polepole huko Donetsk, licha ya hasara kubwa ya binadamu na nyenzo.
Siku ya Jumanne, wanajeshi wa Ukraine katika mkoa huo walisema kulikuwa na mapigano makali katika maeneo ya mijini ya Toretsk na Chasiv Yar, kituo muhimu kimkakati cha kijeshi kwenye mstari wa mbele.
DeepState, kundi la wachambuzi wa masuala ya kijeshi wa Ukraine, linasema kuwa vikosi vya Russia, vimekuwa katikati ya miji hiyo miwili inayogombaniwa kwa miezi kadhaa.
Forum