Mateka walioshikiliwa huko Gaza waliteswa, ikiwemo unyanyasaji wa kingono na kisaikolojia, njaa, kuchomwa na kutopewa matibabu, kulingana na ripoti mpya ya wizara ya afya ya Israel, ambayo itawasilishwa huko Umoja wa Mataifa wiki hii ijayo.
Chad imefanya uchaguzi mkuu Jumapili unaoelezewa na serikali kama hatua muhimu kuelekea kumaliza utawala wa kijeshi, lakini uchaguzi huo umesusiwa na vyama vya upinzani.
Rais wa Azerbaijan Illham Aliyev Jumapili alisema kwamba ndege ya abiria ya nchi yake ambayo ilianguka wiki iliyopita na kuua watu 38, iliharibiwa na shambulizi la risasi kutoka Russia.
Maafisa wa Korea Kusini wamesema takriban watu 179 wamefariki wakati ndege ya abiria ilipoungua Jumapili baada ya kuserereka wakati wa kutua na kugonga uzio wa simenti.
Maelfu ya watu waliandamana Jumamosi katika mji mkuu wa Uturuki Ankara kuomba nyongeza ya kima cha chini cha mshahara, huku wakiimba nyimbo za kuitaka serikali kujiuzulu wakipeperusha bendera za upinzani na taifa.
Rais wa Russia Vladimir Putin Jumamosi amemuomba radhi rais wa Azerbaijan “kwa ajali hiyo mbaya” iliyotokea katika anga ya Russia ambapo ndege ya shirika la ndege la Azerbaijan ilianguka baada ya mifumo ya ulinzi wa anga kutumiwa dhidi ya ndege zisizo na rubani za Ukraine.
Shambulizi la jeshi la Israel lililolenga wanamgambo wa Hamas limesababisha kufungwa kwa hospitali kuu huko kaskazini mwa Gaza na kushikiliwa kwa mkurugenzi wake, shirika la afya duniani na maafisa wa afya wamesema Jumamosi.
Rais wa Kenya William Ruto ameahidi kukomesha vitendo vya utekaji nyara ambavyo vimeongezeka siku za hivi karibuni na kulaaniwa na makundi ya kutetea haki za binadamu, wanasheria na wanasiasa.
Ufaransa imekabidhi kambi yake ya kwanza ya kijeshi kama sehemu ya kujiondoa kijeshi kutoka Chad, majeshi ya Ufaransa na Chad yamesema Alhamisi.
Saa chache baadaye Wa-houthi walifyatua kombora katika uwanja wa ndege Ben Gurion na walirusha Drone kwenye mji wa Tel Aviv
Pyongyang imepeleka maelfu ya wanajeshi kuimarisha jeshi la Russia, ikijumuisha kwenye mkoa wa mpakani wa Kursk
Pandisha zaidi