Mwanajeshi wa Korea Kaskazini aliyekamatwa wakati akipigana katika vita vya Russia dhidi ya Ukraine amefariki kutokana na majeraha aliyoyapata, shirika la ujasusi la Korea Kusini limesema Ijumaa.
Pyongyang imepeleka maelfu ya wanajeshi kuimarisha jeshi la Russia, ikijumuisha kwenye mkoa wa mpakani wa Kursk ambako Ukraine ilifanya mashambulizi ya kushtukiza ya kuvuka mpaka mwezi Agosti.
Mmoja wa wanajeshi hao wa Korea Kaskazini alikamatwa akiwa hai na jeshi la Ukraine siku ya Alhamisi, chanzo cha ujasusi cha Korea Kusini kimeliambia shirika la habari la AFP na kuongeza kuwa eneo alilokamatwa halijulikani.
Saa chache baadaye Idara ya Upelelezi ya Taifa ya Seoul (NIS) ilisema kuwa mwanajeshi huyo alifariki kutokana na majeraha aliyoyapata.
Forum