Jeshi la Sweeden, pia litachangia ndege ya uchunguzi ya ASC 890, serikali imesema katika taarifa.
Walinzi wa pwani wa nchi hiyo watachangia meli nne kusaidia kufuatilia Baltic, na meli saba zaidi zikiwa zimesimama. Sweeden, itakuwa mwanachama wa 32 wa muungano wa kijeshi wa magharibi ifikapo mwezi Machi.
Imeifuata nchi jirani ya Ufini kuingia NATO baada ya Russia, kuanzisha uvamizi kamili kwa Ukraine. Serikali imesema hii itakuwa mara ya kwanza kwa Sweeden, kama mshirika wa NATO kuchangia vikosi vya jeshi katika ulinzi na kulinda umoja huo.
Uamuzi huo umefanyika wakati mfululizo wa matukio katika Baltic yameongeza wasiwasi kuhusu uwezekano wa shughuli za Russia, katika eneo hilo.
Forum