Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 17, 2025 Local time: 02:42

Ukraine imefanya mashambulizi ya ndege zisizo na rubani nchini Russia


Mfano wa ndege zisizotumia rubani-Drone za Russia ambazo zinatumika kwa mashambulizi dhidi ya Ukraine.
Mfano wa ndege zisizotumia rubani-Drone za Russia ambazo zinatumika kwa mashambulizi dhidi ya Ukraine.

Nayo wizara ya Ulinzi ya Russia imesema iliingilia kati na iliharibu ndege zisizokuwa na rubani 85 za Ukraine usiku wa kuamkia leo.

Ukraine ilifanya mashambulizi ya ndege zisizo na rubani kwenye mikoa kadhaa ya Russia, ikishambulia nyumba mbili za makazi katika mkoa wa Tambov na kuwajeruhi angalau watu watatu, Russia ilisema leo Jumamosi.

Mkuu wa mkoa, Evgeny Pervyshov, aliandika ujumbe kwenye mtandao wa Telegram akisema watu walipatiwa matibabu kwa majeraha yaliyotokana na madirisha kuvunjika wakati ndege zisizokuwa na rubani zilipopiga nyumba mbili katika mji wa Kotovsk, takribani kilomita 480 kusini mashariki mwa Moscow.

Alisema majengo hayo yameharibiwa kidogo tu, na wakazi walipewa makazi ya muda, na hawahitajiki kuhama. “Watu watatu walikatwa na vipande vya madirisha yaliyovunjika, wengine wanne walilalamika kuhisi shinikizo la juu la damu, alisema.

Kwingineko wizara ya Ulinzi ya Russia imesema kuwa iliingilia kati na iliharibu ndege zisizokuwa na rubani 85 za Ukraine usiku wa kuamkia leo katika mikoa kadhaa ya nchi, ikijumuisha Drone 31 kwenye Black Sea, 16 kila mmoja katika mikoa ya Voronezh na Krasnodar, na 14 kwenye eneo la Bahari ya Azov.

Shirika la uangalizi wa anga la Russia, Rosaviatsia limesema viwanja vya ndege katika miji ya Kazan, Nizhnekamsk na Ulyanovsk katika mikoa ya Mto Volga imesitisha kwa muda safari za ndege. Kusitishwa kwa safari za ndege katika mji wa Saratov kulitangazwa pia baadaye ili kuhakikisha usalama.

Forum

XS
SM
MD
LG