Rais wa Somalia amekwenda Ethiopia leo Jumamosi, ofisi yake ilisema, ikiwa ishara kubwa zaidi ya kuboresha uhusiano kati ya nchi hizo mbili baada ya mwaka mmoja wa mivutano juu ya mipango ya Addis Ababa kujenga kambi ya jeshi la majini katika mkoa wa Somalia uliojitenga.
Rais Hassan Sheikh Mohamud alisafiri kwenda Ethiopia akitokea Uganda ambako mapema Jumamosi alihudhuria mkutano juu ya kilimo Afrika, ofisi yake ilisema katika taarifa iliyochapishwa kwenye Mtandao wa X.
Akiwa nchini Ethiopia atafanya mazungumzo na uongozi wa Ethiopia ili kuimarisha uhusiano wa nchi hizo mbili na kuendeleza vipaumbele vya pamoja, taarifa hiyo ilisema. “Ushirikiano huu mpya unasisitiza enzi mpya ya ushirikiano kati ya Somalia na Ethiopia”.
Tarehe 2 Januari, Ethiopia pia ilimtuma waziri wake wa ulinzi kwenda Mogadishu, katika ziara ya kwanza ya kiserikali tangu uhusiano kati ya nchi hizo mbili ulipoharibika.
Forum