Mkuu wa usalama wa Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol amesema Jumapili kuwa huenda asishiriki katika juhudi za kumkamata kiongozi aliyeondolewa madarakani katika matamshi ambayo huenda yakasababisha mgogoro wa kisiasa kuelekea kuwepo na malumbano makubwa.
Hati ya kumkamata Yoon kwa misingi ya kufanya uasi inatarajiwa muda wake kumalizika usiku wa manane siku ya Jumatatu kwa saa za Korea Kusini, afisa Park Chong-jun alielezea kuhusu malumbano ya kisheria yanazunguka hati hiyo ikiwa ni sababu ya kutokuwepo kwa ushirikiano.
“Tafadhali achene kutoa matamamshi mabaya ambayo yamepelekea kupunguzwa kwa huduma za ulinzi wa rais kwa jeshi binafsi,” amesema katika taarifa akiongezea kuwa kitengo hicho kimekuwa kikitoa ulinzi kwa marais wote kwa miaka 60, bila ya kujali wameelemea upande gani wa kisiasa.
Maoni hayo yamekuja baada ya mahakama ya Seoul kukataa malalamiko kutoka kwa mawakili wa Yoon kuwa hati ya kutaka kukamatwa kwake haikuwa halali na pia batili, shirika la habari la Yonhap limesema. Mara kadhaa mahakama imepigiwa simu kutoa maoni yao lakini hawakujibu simu.
Forum