Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 07, 2025 Local time: 12:05

Nicolas Sarkozy anatarajiwa kufika mahakamani Jumatatu kwa kesi nyingine


Rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy akionekana kwenye picha iliyochukuliwa kutoka maktaba
Rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy akionekana kwenye picha iliyochukuliwa kutoka maktaba

Wadhifa wa Sarkozy umegubikwa na matatizo ya kisheria tangu aliposhindwa uchaguzi wa rais mwaka 2012.

Rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy tayari amehukumiwa katika kesi mbili tofauti tangu alipoondoka madarakani na siku ya Jumatatu atafika mahakamani kwa kesi ya kukubali fedha haramu kufadhili kampeni yake katika makubaliano na kiongozi wa zamani dikteta Moamer Kadhafi.

Wadhifa wa Sarkozy umegubikwa na matatizo ya kisheria tangu aliposhindwa uchaguzi wa rais mwaka 2012. Lakini alibaku kuwa kiongozi maarufu kwa wengi wa mrengo wa kulia na pia anajulikana kukutana mara kwa mara na Rais Emmanuel Macron.

Mwanasiasa mwenye utashi mkubwa na nguvu, ana miaka 69, na mke wake ni mwana mitindo na muimbaji Carla Bruni, na wakati akiwa madarakani kutoka mwaka 2007 mpaka 2012 alipenda kujulikana kama “rais mwenye hamasa kubwa sana,” amehukumiwa katika kesi mbili, na kushtakiwa katika nyingine na anachunguzwa kuhusiana na nyingine mbili zaidi.

Sarkozy atakuwa kizimbani katika mahakama mjini Paris chini ya nusu mwezi baada ya mahakama ya rufaa ya Ufaransa hapo Desemba 18 kukataa ombi lake la kisheria dhidi ya kifungo cha mwaka mmoja gerezani kwa ushawishi wa kibiashara, ambapo anatakiwa kuvaa kifaa maalum mkononi badala ya kwenda gerezani.

Forum

XS
SM
MD
LG