Moja ya mashambulizi hayo yalipiga kwenye nyumba moja katika eneo la Jabaliya kaskazini mwa Gaza, huku jingine lilipiga kambi ya wakimbizi ya Bureij iliyopo kati-kati ya Ukanda wa Gaza.
Jeshi la Israel halikutoa tamko maoni ya haraka kuhusu mashambulizi hayo, lakini mapema leo Jumatano liliwaonya watu waondoke katika eneo la Bureij, likisema wanamgambo walioko huko walikuwa wakifyatua roketi.
Israel mara kwa mara imekuwa ikiwaambia watu kuhama kutoka sehemu za Gaza katika kile ambacho jeshi linasema ni uhamishaji muhimu kwa ajili ya kutekeleza vita vyake dhidi ya wanamgambo wa Hamas.
Forum