Ouattara alisema Jumanne jioni kwamba Ivory Coast inaweza kujivunia jeshi lake “ambalo uboreshaji wake sasa una ufanisi.”
“Ni katika muktadha huu tumeamua juu ya mchakato wa pamoja na uliopangwa wa kuwaondoa wanajeshi wa Ufaransa nchini kwetu,” Ouattara alitangaza.
Ufaransa imekuwa ikijiandaa kwa miaka mingi kwa kile inachokiita “kujipanga upya” katika uhusiano wa kijeshi baada ya kulazimika kuwaondoa wanajeshi wake huko Mali, Burkina Faso na Niger, ambapo serikali zinazoongozwa na wanajeshi wenye uhasama na nchi hiyo mtawala wa zamani wa kikoloni, walipochukua madaraka katika miaka ya hivi karibuni.
Mwezi Novemba mwaka jana, Senegal na Chad zilitangaza pia kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa kwenye ardhi yao.
Forum