Hatua ya kuondoka wanajeshi wa Ufaransa itaifanya kuwa nchi ya hivi karibuni zaidi kukatiza uhusiano wa kijeshi na taifa hilo lililokuwa utawala wa kikoloni.
Ouattara alisema taifa lake linajivunia jeshi lake ambalo uboreshaji wake wa kisasa unafaa. Akiongeza kuwa ni kupitia uthabiti wake taifa lake limeamua vikosi vya Ufransa viondoke.
Kikosi cha 43 kilichopo katika eneo la Port-Bouet mjini Abidjan -- ambako wanajeshi wa Ufaransa wako huko hivi sasa kitakabidhiwa kwa wanajeshi wa Ivory Coast kuanzia Januari mwaka huu.
Ufaransa imekuwa ikijiandaa kwa miaka mingi kwa kile ilichokitaja kujipanga upya kwa uhusiano wa kijeshi baada ya kualzimishwa kuondoka kwa wanajeshi wake kutoka Mali, Burkina Faso na Niger, ambapo serikali zenye ambazop ziliingia madarakani na kumtaka aliyekuwa mtawala wa zamani wa kikoloni kuondoka.
Mwezi uliopita mataifa ya Senegal na Chad yalitangaza kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa katika ardhi yao.
Forum