Mwaka 2022, idadi ya waathirika ulimwenguni kote iliongezeka kwa asilimia 25, juu zaidi ya viwango vya 2019 kabla ya janga la Covid, Ripoti ya Afisi ya Umoja wa Mataifa kuhusu dawa za kulevya, uhalifu na usafirishaji haramu wa binadamu imesema.
“Wahalifu wanazidi kusafirisha watu na kuwaingiza katika ajira za kulazimishwa, ikiwemo kuwashurutisha kujihusisha na ulaghai wa kisasa wa mtandaoni, huku wanawake na wasichana wakikabiliwa na hatari ya kunyonywa kingono na manyanyaso ya kijinsia,” ilisema ripoti hiyo, ikiongeza kuwa uhalifu wa kupangwa ndio umesababisha zaidi hali hiyo.
Asilimia 38 ya waathirika waliojulikana ni watoto, ikilinganishwa na asilimia 35 kwa takwimu za mwaka 2020 ambazo ndizo msingi wa ripoti ya awali.
Ripoti ya hivi karibuni imeonyesha wanawake watu wazima ni kundi kubwa sana la waathirika, ni sawa na asilimia 39 ya kesi, wakifuatiwa na wanaume kwa asilimia 23, wasichana kwa asilimia 22 na wavulana kwa asilimia 16.
Forum