Ajali hiyo ya mabasi mawili iliyotokea katika barabara ya Daloa-Issia ilisababisha “vifo vya watu 26, 10 kati yao waliungua na moto, na 28 kujeruhiwa”, Oumar Sacko, mkurugenzi mkuu wa usafiri wa barabarani alisema katika taarifa.
Timu ya wizara ilipelekwa kwenye eneo la tukio na uchunguzi umeanzishwa “ kujua sababu za ajali hiyo iliyoua watu wengi,” taarifa hiyo ilisema.
Ajali mbaya za barabarani ni jambo la kawaida nchini Ivory Coast, kutokana na hali mbovu ya baadhi ya barabara na magari, na waendesha pikipiki ambao hawakupasi mtihani wa kuendesha pikipiki.
Forum